32 Walioonewa watakapoona watafurahi;Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
33 Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji,Wala hawadharau wafungwa wake.
34 Mbingu na nchi zimsifu,Bahari na vyote viendavyo ndani yake.
35 Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda,Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.