4 Ikiwa nimemlipa mabayaYeye aliyekaa kwangu salama;(Hasha! Nimemponya yeyeAliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)
5 Basi adui na anifuatie,Na kuikamata nafsi yangu;Naam, aukanyage uzima wangu,Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
6 BWANA uondoke kwa hasira yako;Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu;Uamke kwa ajili yangu;Umeamuru hukumu.
7 Kusanyiko la mataifa na likuzunguke,Na juu yake uketi utawale.
8 BWANA atawaamua mataifa,BWANA, unihukumu mimi,Kwa kadiri ya haki yangu,Sawasawa na unyofu nilio nao.
9 Ubaya wao wasio haki na ukome,Lakini umthibitishe mwenye haki.Kwa maana mjaribu mioyo na viunoNdiye Mungu aliye mwenye haki.
10 Ngao yangu ina Mungu,Awaokoaye wanyofu wa moyo.