11 Wakisema, Mungu amemwacha,Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.
12 Ee Mungu, usiwe mbali nami;Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.
13 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu.Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
14 Nami nitatumaini daima,Nitazidi kuongeza sifa zake zote.
15 Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wakoMchana kutwa; maana sijui hesabu yake.
16 Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU;Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.
17 Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu;Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.