20 Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya,Utatuhuisha tena.Utatupandisha juu tenaTokea pande za chini ya nchi.
21 Laiti ungeniongezea ukuu!Urejee tena na kunifariji moyo.
22 Nami nitakushukuru kwa kinanda,Na kweli yako, Ee Mungu wangu.Nitakuimbia Wewe kwa kinubi,Ee Mtakatifu wa Israeli.
23 Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo,Na nafsi yangu uliyoikomboa.