9 Usinitupe wakati wa uzee,Nguvu zangu zipungukapo usiniache.
10 Kwa maana adui zangu wananiamba,Nao wanaoniotea roho yangu hushauriana.
11 Wakisema, Mungu amemwacha,Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.
12 Ee Mungu, usiwe mbali nami;Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.
13 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu.Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
14 Nami nitatumaini daima,Nitazidi kuongeza sifa zake zote.
15 Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wakoMchana kutwa; maana sijui hesabu yake.