1 Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako,Na mwana wa mfalme haki yako.
2 Atawaamua watu wako kwa haki,Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
3 Milima itawazalia watu amani,Na vilima navyo kwa haki.
4 Atawahukumu walioonewa wa watu,Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea.
5 Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua,Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi.
6 Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa,Kama manyunyu yainyweshayo nchi.
7 Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.