17 Jina lake na lidumu milele,Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;Mataifa yote na wajibariki katika yeye,Na kumwita heri.
18 Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli,Atendaye miujiza Yeye peke yake;
19 Jina lake tukufu na lihimidiwe milele;Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.
20 Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha.