7 Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.
8 Na awe na enzi toka bahari hata bahari,Toka Mto hata miisho ya dunia.
9 Wakaao jangwani na wainame mbele zake;Adui zake na warambe mavumbi.
10 Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi;Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
11 Naam, wafalme wote na wamsujudie;Na mataifa yote wamtumikie.
12 Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo,Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.
13 Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,Na nafsi za wahitaji ataziokoa.