1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,Kwa hao walio safi mioyo yao.
2 Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka,Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.
3 Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna,Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.
4 Maana hawana maumivu katika kufa kwao,Na mwili wao una nguvu.
5 Katika taabu ya watu hawamo,Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.
6 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao,Jeuri huwavika kama nguo.
7 Macho yao hutokeza kwa kunenepa,Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.