11 Nao husema, Mungu ajuaje?Yako maarifa kwake aliye juu?
12 Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki,Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.
13 Hakika nimejisafisha moyo wangu bure,Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.
14 Maana mchana kutwa nimepigwa,Na kuadhibiwa kila asubuhi.
15 Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo;Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.
16 Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo;Ikawa taabu machoni pangu;
17 Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu,Nikautafakari mwisho wao.