13 Hakika nimejisafisha moyo wangu bure,Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.
14 Maana mchana kutwa nimepigwa,Na kuadhibiwa kila asubuhi.
15 Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo;Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.
16 Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo;Ikawa taabu machoni pangu;
17 Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu,Nikautafakari mwisho wao.
18 Hakika Wewe huwaweka penye utelezi,Huwaangusha mpaka palipoharibika.
19 Namna gani wamekuwa ukiwa mara!Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.