24 Utaniongoza kwa shauri lako,Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
25 Ni nani niliye naye mbinguni,Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.
26 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka,Bali Mungu ni mwamba wa moyo wanguNa sehemu yangu milele.
27 Maana wajitengao nawe watapotea;Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.