4 Maana hawana maumivu katika kufa kwao,Na mwili wao una nguvu.
5 Katika taabu ya watu hawamo,Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.
6 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao,Jeuri huwavika kama nguo.
7 Macho yao hutokeza kwa kunenepa,Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.
8 Hudhihaki, husimulia mabaya,Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.
9 Wameweka kinywa chao mbinguni,Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.
10 Kwa hiyo watu wake hugeuka huko,Na maji yaliyojaa humezwa nao.