1 Ee Mungu, mbona umetutupa milele?Kwa nini hasira yako inatoka moshiJuu ya kondoo wa malisho yako?
2 Ulikumbuke kusanyiko lako,Ulilolinunua zamani.Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako,Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.
3 Upainulie miguu yako palipoharibika milele;Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.
4 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;Wameweka bendera zao ziwe alama.
5 Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,Waikate miti ya msituni.