4 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;Wameweka bendera zao ziwe alama.
5 Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,Waikate miti ya msituni.
6 Na sasa nakishi yake yote piaWanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo.
7 Wamepatia moto patakatifu pako;Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.
8 Walisema mioyoni mwao,Na tuwaangamize kabisa;Mahali penye mikutano ya MunguWamepachoma moto katika nchi pia.
9 Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii,Wala kwetu hakuna ajuaye, hata lini?
10 Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini?Adui alidharau jina lako hata milele?