12 Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,Katika nchi ya Misri, konde la Soani.
13 Aliipasua bahari akawavusha;Aliyasimamisha maji mfano wa chungu.
14 Akawaongoza kwa wingu mchana,Na usiku kucha kwa nuru ya moto.
15 Akapasua miamba jangwani;Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi.
16 Akatokeza na vijito gengeni,Akatelemsha maji kama mito.
17 Lakini wakazidi kumtenda dhambi,Walipomwasi Aliye juu katika nchi ya kiu.
18 Wakamjaribu Mungu mioyoni mwaoKwa kutaka chakula kwa tamaa zao.