24 Akawanyeshea mana ili wale;Akawapa nafaka ya mbinguni.
25 Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.
26 Aliuelekeza upepo wa mashariki mbinguni;Akaiongoza kusi kwa uweza wake.
27 Akawanyeshea nyama kama mavumbi,Na ndege wenye mbawa,Kama mchanga wa bahari.
28 Akawaangusha kati ya matuo yao,Pande zote za maskani zao.
29 Wakala wakashiba sana;Maana aliwaletea walivyovitamani;
30 Hawakuachana na matakwa yao.Ila chakula chao kikali ki vinywani mwao