31 Hasira ya Mungu ikapanda juu yao,Akawaua waliokuwa wanono;Akawaangusha chini vijana wa Israeli.
32 Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi,Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.
33 Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi,Na miaka yao kwa hofu ya kuwasitusha.
34 Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta;Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.
35 Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao,Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao.
36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.
37 Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.