35 Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao,Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao.
36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.
37 Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
38 Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema,Husamehe uovu wala haangamizi.Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake,Wala haiwashi hasira yake yote.
39 Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili,Upepo upitao wala haurudi.
40 Walimwasi jangwani mara ngapi?Na kumhuzunisha nyikani!
41 Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu;Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.