48 Akaacha ng’ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe,Na makundi yao kwa umeme.
49 Akawapelekea ukali wa hasira yake,Ghadhabu, na uchungu, na taabu,Kundi la malaika waletao mabaya.
50 Akiifanyizia njia hasira yake;Wala hakuziepusha roho zao na mauti,Bali aliiachia tauni uhai wao;
51 Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri,Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu.
52 Bali aliwaongoza watu wake kama kondoo,Akawachunga kama kundi jangwani.
53 Hao akawachukua salama wala hawakuogopa,Bali bahari iliwafunikiza adui zao.
54 Akawapeleka hadi mpaka wake mtakatifu,Mlima alioununua kwa mkono wake wa kuume.