52 Bali aliwaongoza watu wake kama kondoo,Akawachunga kama kundi jangwani.
53 Hao akawachukua salama wala hawakuogopa,Bali bahari iliwafunikiza adui zao.
54 Akawapeleka hadi mpaka wake mtakatifu,Mlima alioununua kwa mkono wake wa kuume.
55 Akawafukuza mataifa mbele yao,Akawapimia urithi kwa kamba,Na kuwakalisha kabila za Israeli katika hema zao.
56 Lakini walimjaribu Mungu Aliye juu, wakamwasi,Wala hawakuzishika shuhuda zake.
57 Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao;Wakaepea kama upinde usiofaa.
58 Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu,Wakamtia wivu kwa sanamu zao.