59 Mungu akasikia, akaghadhibika,Akamkataa Israeli kabisa.
60 Akaiacha maskani ya Shilo,Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu;
61 Akaziacha nguvu zake kutekwa,Na fahari yake mkononi mwa mtesi.
62 Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga;Akaughadhibikia urithi wake.
63 Moto ukawala vijana wao,Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,
64 Makuhani wao walianguka kwa upanga,Wala wajane wao hawakuomboleza.
65 Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi,Kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo;