1 Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,Wamelinajisi hekalu lako takatifu.Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.
2 Wameziacha maiti za watumishi wakoZiwe chakula cha ndege wa angani.Na miili ya watauwa wakoIwe chakula cha wanyama wa nchi.
3 Wamemwaga damu yao kama majiPande zote za Yerusalemu,Wala hapakuwa na mzishi.
4 Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.