3 Wamemwaga damu yao kama majiPande zote za Yerusalemu,Wala hapakuwa na mzishi.
4 Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
5 Ee BWANA, hata lini? Utaona hasira milele?Wivu wako utawaka kama moto?
6 Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua,Na falme za hao wasioliitia jina lako.
7 Kwa maana wamemla Yakobo,Na matuo yake wameyaharibu.
8 Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,Rehema zako zije kutulaki hima,Kwa maana tumedhilika sana.
9 Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,Kwa ajili ya jina lako.