1 Wewe uchungaye Israeli, usikie,Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi;Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
2 Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,Uziamshe nguvu zako,Uje, utuokoe.
3 Ee Mungu, uturudishe,Uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
4 Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hata liniUtayaghadhibikia maombi ya watu wako?
5 Umewalisha mkate wa machozi,Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu.
6 Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.
7 Ee Mungu wa majeshi, uturudishe,Uangazishe uso wako nasi tutaokoka.