13 Nguruwe wa msituni wanauharibu,Na hayawani wa kondeni wanautafuna.
14 Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu.
15 Na mche ule ulioupandaKwa mkono wako wa kuume;Na tawi lile ulilolifanyaKuwa imara kwa nafsi yako.
16 Umechomwa moto; umekatwa;Kwa lawama ya uso wako wanapotea.
17 Mkono wako na uwe juu yakeMtu wa mkono wako wa kuume;Juu ya mwanadamu uliyemfanyaKuwa imara kwa nafsi yako;
18 Basi hatutakuacha kwa kurudi nyuma;Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.