4 Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hata liniUtayaghadhibikia maombi ya watu wako?
5 Umewalisha mkate wa machozi,Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu.
6 Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.
7 Ee Mungu wa majeshi, uturudishe,Uangazishe uso wako nasi tutaokoka.
8 Ulileta mzabibu kutoka Misri,Ukawafukuza mataifa ukaupanda.
9 Ulitengeneza nafasi mbele yake,Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi.
10 Milima ilifunikwa kwa uvuli wake,Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu.