1 Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha,Mshangilieni Mungu wa Yakobo.
2 Pazeni zaburi, pigeni matari,Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi,Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
4 Kwa maana ni sheria kwa Israeli,Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
5 Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu,Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;Maneno yake nisiyemjua naliyasikia.
6 Nimelitenga bega lake na mzigo,Mikono yake ikaachana na kikapu.
7 Katika shida uliniita nikakuokoa;Nalikuitikia katika sitara ya radi;Nalikujaribu penye maji ya Meriba.