4 Kwa maana ni sheria kwa Israeli,Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
5 Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu,Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;Maneno yake nisiyemjua naliyasikia.
6 Nimelitenga bega lake na mzigo,Mikono yake ikaachana na kikapu.
7 Katika shida uliniita nikakuokoa;Nalikuitikia katika sitara ya radi;Nalikujaribu penye maji ya Meriba.
8 Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya,Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;
9 Usiwe na mungu mgeni ndani yako;Wala usimsujudie mungu mwingine.
10 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,Niliyekupandisha toka nchi ya Misri;Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.