1 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;Katikati ya miungu anahukumu.
2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma,Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima;Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4 Mwokoeni maskini na mhitaji;Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;Misingi yote ya nchi imetikisika.
6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu,Na wana wa Aliye juu, nyote pia.