1 Ee Mungu, usistarehe,Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.
2 Maana adui zako wanafanya ghasia,Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao.
3 Juu ya watu wako wanafanya hila,Na kushauriana juu yao uliowaficha.
4 Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa,Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.
5 Maana wanashauriana kwa moyo mmoja,Juu yako wanafanyana agano.
6 Hema za Edomu, na Waishmaeli,Na Moabu, na Wahagari,
7 Gebali, na Amoni, na Amaleki,Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,