11 Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna.
12 Ambao Walisema,Na tutamalaki makao ya Mungu.
13 Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli,Mithili ya makapi mbele ya upepo,
14 Kama moto uteketezao msitu,Kama miali ya moto iiwashayo milima,
15 Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako,Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16 Uwajaze nyuso zao fedheha;Wakalitafute jina lako, BWANA.
17 Waaibike, wafadhaike milele,Naam, watahayarike na kupotea.