4 Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa,Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.
5 Maana wanashauriana kwa moyo mmoja,Juu yako wanafanyana agano.
6 Hema za Edomu, na Waishmaeli,Na Moabu, na Wahagari,
7 Gebali, na Amoni, na Amaleki,Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,
8 Ashuri naye amepatana nao,Wamewasaidia wana wa Lutu.
9 Uwatende kama Midiani, kama Sisera,Kama Yabini, penye kijito Kishoni.
10 Ambao waliangamizwa Endori;Wakawa samadi juu ya nchi.