6 Hema za Edomu, na Waishmaeli,Na Moabu, na Wahagari,
7 Gebali, na Amoni, na Amaleki,Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,
8 Ashuri naye amepatana nao,Wamewasaidia wana wa Lutu.
9 Uwatende kama Midiani, kama Sisera,Kama Yabini, penye kijito Kishoni.
10 Ambao waliangamizwa Endori;Wakawa samadi juu ya nchi.
11 Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna.
12 Ambao Walisema,Na tutamalaki makao ya Mungu.