1 BWANA, umeiridhia nchi yako,Umewarejeza mateka wa Yakobo.
2 Umeusamehe uovu wa watu wako,Umezisitiri hatia zao zote.
3 Umeiondoa ghadhabu yako yote,Umerudi na kuuacha ukali wa hasira yako.
4 Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
5 Je! Utatufanyia hasira hata milele?Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi?