4 Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
5 Je! Utatufanyia hasira hata milele?Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi?
6 Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha,Watu wako wakufurahie?
7 Ee BWANA, utuonyeshe rehema zako,Utupe wokovu wako.
8 Na nisikie atakavyosema Mungu BWANA,Maana atawaambia watu wake amani,Naam, na watauwa wake pia,Bali wasiurudie upumbavu tena.
9 Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,Utukufu ukae katika nchi yetu.
10 Fadhili na kweli zimekutana,Haki na amani zimehusiana.