3 Wewe, Bwana, unifadhili,Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.
4 Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.
5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,Umekuwa tayari kusamehe,Na mwingi wa fadhili,Kwa watu wote wakuitao.
6 Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;Uisikilize sauti ya dua zangu.
7 Siku ya mateso yangu nitakuita,Kwa maana utaniitikia.
8 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,Wala matendo mfano wa matendo yako.
9 Mataifa yote uliowafanya watakuja;Watakusujudia Wewe, Bwana,Watalitukuza jina lako;