1 Ee BWANA, Mungu wa wokovu wanguMchana na usiku nimelia mbele zako.
2 Maombi yangu yafike mbele zako,Uutegee ukelele wangu sikio lako.
3 Maana nafsi yangu imeshiba taabu,Na uhai wangu umekaribia kuzimu.
4 Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni;Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.
5 Miongoni mwao waliokufa nimetupwa,Kama waliouawa walalao makaburini.Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,Wametengwa mbali na mkono wako.