14 BWANA, kwa nini kuitupa nafsi yangu,Na kunificha uso wako?
15 Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana,Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.
16 Hasira zako kali zimepita juu yangu,Maogofyo yako yameniangamiza.
17 Yamenizunguka kama maji mchana kutwa,Yamenisonga yote pamoja.