1 Fadhili za BWANA nitaziimba milele;Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
2 Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
3 Nimefanya agano na mteule wangu,Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.
4 Wazao wako nitawafanya imara milele,Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.
5 Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako,Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.
6 Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA?Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika?
7 Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu,Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.