14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako,Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
15 Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,Ee BWANA, huenenda katika nuru ya uso wako.
16 Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,Na kwa haki yako hutukuzwa.
17 Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.
18 Maana ngao yetu ina BWANA,Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.
19 Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi,Ukasema, nimempa aliye hodari msaada;Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,Nimempaka mafuta yangu matakatifu.