16 Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,Na kwa haki yako hutukuzwa.
17 Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.
18 Maana ngao yetu ina BWANA,Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.
19 Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi,Ukasema, nimempa aliye hodari msaada;Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake,Na mkono wangu utamtia nguvu.
22 Adui hatamwonea,Wala mwana wa uovu hatamtesa.