18 Maana ngao yetu ina BWANA,Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.
19 Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi,Ukasema, nimempa aliye hodari msaada;Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake,Na mkono wangu utamtia nguvu.
22 Adui hatamwonea,Wala mwana wa uovu hatamtesa.
23 Bali nitawaponda watesi wake mbele yake,Nitawapiga wanaomchukia.
24 Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo,Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.