24 Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo,Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.
25 Nitaweka mkono wake juu ya bahari,Na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26 Yeye ataniita, Wewe baba yangu,Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
27 Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza,Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.
28 Hata milele nitamwekea fadhili zangu,Na agano langu litafanyika amini kwake.
29 Wazao wake nao nitawadumisha milele,Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.
30 Wanawe wakiiacha sheria yangu,Wasiende katika hukumu zangu,