28 Hata milele nitamwekea fadhili zangu,Na agano langu litafanyika amini kwake.
29 Wazao wake nao nitawadumisha milele,Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.
30 Wanawe wakiiacha sheria yangu,Wasiende katika hukumu zangu,
31 Wakizihalifu amri zangu,Wasiyashike maagizo yangu,
32 Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo,Na uovu wao kwa mapigo.
33 Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye,Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.
34 Mimi sitalihalifu agano langu,Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu.