31 Wakizihalifu amri zangu,Wasiyashike maagizo yangu,
32 Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo,Na uovu wao kwa mapigo.
33 Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye,Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.
34 Mimi sitalihalifu agano langu,Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu.
35 Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu,Hakika sitamwambia Daudi uongo,
36 Wazao wake watadumu milele,Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu.
37 Kitathibitika milele kama mwezi;Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.