36 Wazao wake watadumu milele,Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu.
37 Kitathibitika milele kama mwezi;Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.
38 Walakini Wewe umemtupa na kumkataa,Umemghadhibikia masihi wako.
39 Umechukizwa na agano la mtumishi wako,Umeinajisi taji yake na kuitupa chini.
40 Umeyabomoa maboma yake yote,Umezifanya ngome zake kuwa magofu.
41 Wote wapitao njiani wanateka mali zake;Amekuwa laumu kwa jirani zake;
42 Umeutukuza mkono wa kuume wa watesi wake;Umewafurahisha wote wanaomchukia.