39 Umechukizwa na agano la mtumishi wako,Umeinajisi taji yake na kuitupa chini.
40 Umeyabomoa maboma yake yote,Umezifanya ngome zake kuwa magofu.
41 Wote wapitao njiani wanateka mali zake;Amekuwa laumu kwa jirani zake;
42 Umeutukuza mkono wa kuume wa watesi wake;Umewafurahisha wote wanaomchukia.
43 Pia umeurudisha nyuma ukali wa upanga wake;Wala hukumsimamisha vitani.
44 Umeikomesha fahari yake;Kiti chake cha enzi umekitupa chini.
45 Umezipunguza siku za ujana wake;Umemvika aibu.