41 Wote wapitao njiani wanateka mali zake;Amekuwa laumu kwa jirani zake;
42 Umeutukuza mkono wa kuume wa watesi wake;Umewafurahisha wote wanaomchukia.
43 Pia umeurudisha nyuma ukali wa upanga wake;Wala hukumsimamisha vitani.
44 Umeikomesha fahari yake;Kiti chake cha enzi umekitupa chini.
45 Umezipunguza siku za ujana wake;Umemvika aibu.
46 Ee BWANA, hata lini? Utajificha hata milele?Ghadhabu yako itawaka kama moto?
47 Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu;Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!