44 Umeikomesha fahari yake;Kiti chake cha enzi umekitupa chini.
45 Umezipunguza siku za ujana wake;Umemvika aibu.
46 Ee BWANA, hata lini? Utajificha hata milele?Ghadhabu yako itawaka kama moto?
47 Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu;Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!
48 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti,Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?
49 Bwana, zi wapi fadhili zako za kwanza,Ulizomwapia Daudi kwa uaminifu wako?
50 Ee Bwana, ukumbuke,Wanavyosimangwa watumishi wako;Jinsi ninavyostahimili kifuani mwanguMasimango ya watu wengi.